Wasafi TV yapigwa stop kwa miezi sita

0
121

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha Television cha Wasafi TV kwa muda wa miezi sita, kutokana na kukiuka kanuni namba 11(1) (a)(b) na c za kanuni za mawasiliano ya kieletoniki na posta mwaka 2018, yanayomtaka kuzingatia maudhui.

Inadaiwa kuwa, Januari Mosi mwaka huu majira ya saa 2 hadi saa 5 usiku kupitia kipindi cha Tumewasha Live Concert, Wasafi TV ilirusha maudhui jongefu yakimwonesha Msanii Gift Mwakyusa maarufu kama Giggy Money akicheza katika jukwaa huku akionesha utupu wa mwili wake kinyume na kanuni hizo.