Wanunuzi wa Pamba Katavi wapewa siku 14 kulipa pesa za Wakulima

0
217

Serikali imetoa muda wa siku 14 kwa Wanunuzi wote walionunua pamba ya Wakulima kwa mkopo mkoani Katavi, kulipa pesa hizo.

Amesema kuwa, haiwezekani Wakulima hao wahangaike kulima Pamba hiyo kwa tabu na watu wengine wajitokeze na kuinunua kwa mkopo.

Rais Magufuli ametoa muda huo huko Mpanda mkoani Katavi, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na Wakazi wa mkoa huo, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Amemuagiza Waziri wa Kilimo, – Japhet Hasunga na Mkuu wa mkoa wa Katavi Juma Homerra, kukakikisha malipo hayo yanafanyika ndani ya siku hizo 14 ili Wakulima hao waweze kutumia fedha hizo kwa malengo waliojiwekea.

Hata hivyo Rais Magufuli ameagiza kuwa, kwa Pamba ambayo bado iko kwa Wakulima isinunuliwe kwa mkopo, bali kwa pesa taslimu.

Amewaahidi Wakulima wa Pamba mkoani Katavi kuwajengea vinu vya kuchambua Pamba kwa fedha za Serikali.