Wanne wauawa, sita wajeruhiwa katika shambulio Dar

0
434

Watu wanne wameuawa wakiwemo askari polisi watatu na askari mmoja wa kampuni ya ulinzi ya SGA katika tukio la majibizano ya risasi na mtu mmoja ambaye jina lake halijafahamika lililotokea pembezoni mwa ubalozi wa Ufaransa mkoani Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea majira ya mchana ambapo mtu aliyefanya mauaji hayo pia amepigwa risasi na kufariki dunia papohapo.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi Nchini Kamishna Liberatus Sabas amesema Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini uraia wa mtu huyo na kwa nini ameamua kufanya tukio hilo.

Kamishna Sabas amesema askari wengine sita wamejeruhiwa katika tukio hilo ambalo bado Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza chanzo chake.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi ili kudhibiti matukio kama hayo yasitokee tena