Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kutumia mitandao ya kijamii kueneza uvumi wa vifo vya watu wakidai wamefariki kwa maambukizi ya virusi vya Corona.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema uzushi huo umewatia hofu na taharuki wananchi.
Akizungumzia tukio hilo amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni hao ni Frank Nyange (47), Mozes Mgao (34) Mohamedi Lutambi (47) na Bumija Senkondo (55).
“Watuhumiwa hawa wanne tuliowakamata na wengine ambao tunaendelea kuwatafuta wanasambaza taarifa za uvumi za vifo vya watu wakidai wamekufa kwa Corona na pia wanapendekeza majina ya viongozi wa Serikali ambao walitamani wafe haraka kwa Corona,” ameelza Kamanda Nyigesa.
