Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Mama Shamim Khan amesema sensa ya watu na makazi itakayofanyika Agosti 28 mwaka huu ni muhimu kwa Taifa, hivyo amewahamasisha wanawake kutoa ushirikiano kufanikisha zoezi hilo.
Mama Khan ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa kongamano la viongozi wa dini kuhusu sensa ya watu na makazi.
Amesema wanawake wameendelea kupewa nafasi mbalimbali za uongozi, hivyo wanapaswa kuonesha mfano wa kuwajibika katika kusimamia mipango ya maendeleo ambapo sensa ya watu na makazi itasaidia kufanikisha mipango hiyo.