Wanawake kote nchini wametakiwa kuwekeza na kuangalia fursa zilizopo katika sekta ya madini ili kujiongezea kipato chao.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko alipokuwa akihitimisha hotuba yake na kufunga mkutano wa kimataifa wa wadau sekta ya madini nchini Tanzania.
Waziri Biteko amesisitiza kuwa wachimbaji wadogo na wawekezaji katika sekta hiyo watumie fursa ya makongamano, mikutano na viongozi wao ili kuboresha na kuimarisha sekta hiyo.