Facebook Instagram Twitter Youtube
  • Home
  • Kuhusu TBC
    • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
    • Privacy Policy
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Burudani
  • Biashara
  • Tuzo
  • Live Stream
    • TBC1
    • TBC2
Search
. .
  • Home
  • Kuhusu TBC
    • MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA
    • Privacy Policy
  • Kitaifa
  • Kimataifa
  • Michezo
  • Burudani
  • Biashara
  • Tuzo
  • Live Stream
    • TBC1
    • TBC2
Home Kitaifa Wanawake wajasiriamali wapewa elimu ya utunzaji fedha
  • Kitaifa

Wanawake wajasiriamali wapewa elimu ya utunzaji fedha

By
Rose Shayo
-
November 24, 2020
0
772
Share
Facebook
Twitter
WhatsApp
Linkedin

    Wajasiriamali mkoani Kigoma wametakiwa kuzitumia taasisi za kifedha kupata taarifa mbalimbali za mikopo, kutunza akiba pamoja na kufahamu namna ya kutunza kumbukumbu ili waweze kuendeleza biashara zao na kujikwamua kiuchumi.

    Akizungumza kwa nyakati tofauti katika wilaya za Bihigwe na Kigoma, Meneja wa CRDB kanda ya magharibi, Said Pamui amesema ni muhimu kwa wajasiriamali kuwa na mpango maalum wa utendaji utakaochochewa na utunzaji wa kumbukumbu za matumizi sahihi ya fedha kwa kuzingatia vpaumbele vya maendeleo.

    Semina hiyo ambayo imewakutanisha wajasiriamali wanawake kwa nyakati tofauti katika wilaya ya Buhigwe pamoja na Manispaa ya Kigoma ujiji imekuwa na manufaa makubwa ambapo baadhi ya wajasiliamali wamesema mpango huo utakuwa na msaada kwao ikiwemo kuepukana na changamoto ya ukosefu wa mitaji, utunzani wa kumbukumbu na utafutaji wa masoko.

    Pamui akaongeza kuwa, “Benki ya CRDB inaamini kwamba kumjuza na kumuelekeza mwanamke katika fani mbalimbali za ujasiliamali itakuwa imefanikiwa kuliendeleza Taifa kwa kiwango kikubwa kiuchumi.’’

    Mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wanawake kiuchumi CRDB, Rachel Senni amesema lengo ni kumuinua mwanamke kiuchumi kwa kumpatia elimu ya kupata mikopo, kutunza akiba pamoja na kufahamu namna ya kutunza kumbukumbu ambapo akaunti ya malkia imeelezwa kuwa suluhisho la changamoto kwa wajasiliamali wanawake.

    • TAGS
    • crdb
    • malkia account
    • Wajasiriamali
    • wanawake wajasiriamali
    Facebook
    Twitter
    WhatsApp
    Linkedin
      Previous articleWabunge 19 wa Viti Maalumu CHADEMA waapishwa
      Next articleSCOATLAND: Nchi ya kwanza duniani kutoa taulo za hedhi bure
      Rose Shayo
      Sign in
      Welcome! Log into your account
      Forgot your password? Get help
      Password recovery
      Recover your password
      A password will be e-mailed to you.
      © Newspaper WordPress Theme by TagDiv
      Skip to toolbar
      • About WordPress
        • WordPress.org
        • Documentation
        • Support
        • Feedback
      • Log In