Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa amewataka wanawake kuacha kutumika kwa lengo la kupata vyeo ama kazi katika taasisi zozote nchini.
Naibu Waziri Mwanjelwa ameyasema hayo katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Tbc ambapo amesema mwanamke ni hekalu takatifu na si mashine ya kumfurahisha mtu mwingine bila makubaliano.
Amesema mwanamke yeyote anayefanyiwa hivyo ahakikishe anaripoti suala hili katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa hatua zaidi.