Wanawake Ulanga walalamikia Chagulaga

0
138

Mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Ngollo Malenya amepiga marufuku tabia ya baadhi ya vijana kutoka jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma
kuwalazimisha wanawake kufanya nao mapenzi kwa nguvu na kutaka kuwaoa bila ridhaa yao.

Ngollo ametoa Kauli hiyo katika kijiji cha Igumbiro ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ulanga.

Amesema mila hizo za kuwataka wanawake kwa nguvu maarufu kwa jina la Chagulaga zimepitwa na wakati, hivyo ni vema zikaachwa.

Mkuu hiuyo wa wilaya ya Ulanga amelazimika kitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wanawake wilayani humo kulalamika kuwa kuna baadhi ya wanaume wanawalazimisha kufanya nao mapenzi ama kuwaoa bila ridhaa yao na hufanya hivyo kwa kuwavizia wakiwa wanakwenda shambani au wakiwa kwenye minada.

Wamedai kuwa Wanaume hao wakikutana na mwanamke humzunguka na kumwambia achague mtu mmoja afanye nae mapenzi na akikataa analazimishwa na akikataa anachapwa viboko na kama kuna baba ama mwenza wake anakuja kumsaidia naye anachapwa viboko.

Ngollo amesema tabia hiyo ni udhalilishaji na kwamba serikali haitafumbia macho mtu au kikundi cha watu wenye tabia hiyo