Wanaume wengi wanatafuna vibaya

0
283

Mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya kijamii wa TBC FM, Mariam Migomba amesema wanaume wengi hawajui namna ya kutafuna vyakula mbele za watu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Wikiendi kilichokuwa kikijadili nafasi ya jamii katika malezi ya watoto, Miriam amesema tatizo hilo linatokana na malezi waliyopata kutoka kwenye familia zao tangu wakiwa watoto.

“Mpaka leo kuna wanaume wanatafuna vibaya, lakini ni kwa sababu gani, hakuambiwa we acha, we hiyo mwiko,” amesema Mariam.

Ameeleza kwamba ni wajibu wazazi na walezi kuwafundisha watoto tabia njema, kwani tabia wanakuwa nazo hivyo kuzitumia ukubwani.

“…..Akishafika sasa ule umri amevunja ungo ama amebalehe anaitwa mtu, mimi ni Mkurya lakini nimekulia huku Pwani, mtoto ana Nyakanga akiwa binti unampeleka kwa Nyakanga, watu walichukulia dhana ya kumpeleka mtoto kwa Nyakanga anakwenda kufundishwa vibaya, kwa sababu kuna Nyakanga, Kungwi na Somo….” ameongeza Mariam.