Wanaume Tanga washauriwa kupima afya

0
290

Mkuu wa mkoa wa Tanga, – Martine Shigela amewashauri Wanaume wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kupima afya zao, badala ya kutegemea majibu ya afya zao kutoka katika vipimo vya wenza wao pindi wanapopata ujauzito.

Shigela ametoa ushauri huo jijini Tanga wakati wa uzinduzi wa mradi wa Afya Kamilifu.

Amesema kuwa kumekua na tabia kwa baadhi ya akina Wanaume mkoani Tanga kutopima afya zao ili kujua kama wana maambukizi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi au la, hali inayochangia kuendelea kuenea kwa virusi hivyo.