Rais Samia Suluhu Hassan amezielekeza mamlaka husika kufuatilia mtindo wa sasa unaofanyika kwenye baadhi ya karakana za kutengeneza magari ambapo mafundi hutoa unga unaopatikana kwenye exhaust za magari il kufanikisha utengenezaji wa dawa za kulevya.
Rais Samia ameyasema hayo mkoani Arusha alipokuwa akihitimisha maadhimisho ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani kitaifa.
“Sasa hivi kuna mtindo wanapasua exhaust za magari zile….. yale yanayotoa moshi ndani yake kule kuna unga fulani unaosababisha control ya ule moshi, sasa ule unga unatolewa kwenye gereji zetu huko… unatolewa unakwenda kuchanganywa na haya maunga vijana wetu wanaotumia”.
“Unga unaotoka kwenye exhaust ni sumu kubwa sasa ukichangangwa na unga huu wanaotumia wakijidunga, ndio maana unasikia hawa mateja wanaanguka wanakufa kwa sababu ya sumu hiyo wanayojipiga….., Sasa hili sijui la mamlaka ipi hapa lakini niombe mamlaka zote za Serikali zinazohusika kwenda kuangalia hili”.