Wanaowatumia Watu wenye Ulemavu kama mtaji wasakwa

0
149

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikiila Wamiliki watano wa nyumba za wageni kwa kuhuma za kuwahifadhi Watu wenye ulemavu na kuwatumikisha kazi za ombaomba katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni Filipina Swai, ambaye ni mmiliki wa nyumba ya wageni  ijulikanayo kama Kibosi, huku eneo la Tandale Uziuri likitajwa kukithiri kwa vitendo hibyo.

Filipina ameamua kujisalishamisha mwenyewe Polisi baada ya nyumba yake ya wageni kukutwa  imehifadhi Watu wenye Ulemavu, ambao walikuwa wakitumikishwa kazi za ombaomba.

Mbali na kujisalimisha Polisi, Filipina pia amekuatana na kufanya mazungumzo na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu Ummy Nderiananga, kuhusu jambo hilo.

Hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari nchini vilitangaza taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Wamiliki wa nyumba za wageni wanaotuhumiwa kuwahifadhi Watu wenye ulemavu na kuwatumikisha kazi za ombaomba kama mtaji, taarifa zilizovuta hisia za watu wengi.