Wanaotumia jina la Waziri Mkuu kutapeli wasakwa

0
263

Wananchi wametakiwa kujihadhari na ujumbe unaosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook unaotumia jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ujumbe unaowataka wajasiriamali watume pesa ili wapewe mkopo na taasisi iliyojitambulisha kama Kassim Majaliwa Foundation.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma, imekanusha kuwepo kwa taasisi hiyo na kusema kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hana na wala hahusiki na taasisi yoyote ya utoaji wa mikopo.

Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia suala hilo ili wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria.

Wananchi wengi wamedai kutumiwa ujumbe unaowataka watume namba za vitambulisho vyao vya kupigia kura ili waweze kupatiwa mkopo ndani ya saa 24 kwa kutumia namba 0652940 415, ambayo imesajiliwa kwa jina la Yunus Milanzi.