Wanaopandisha bei za vitakasa mikono na barakoa kunyang’anywa leseni

0
220

Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa ameagiza kunyang’anywa leseni maduka yote ya dawa yaliyopandisha maradufu bei za barakoa (Mask) na vitakasa mikono (Sanitizers), baada ya kuingia nchini kwa virusi vya corona.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo baada ya kukagua bei za bidhaa hizo katika duka la dawa la Nakiete jijini Dar es salaam na kukuta bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya juu.

Pia Waziri Bashungwa ameagiza kuhojiwa kwa mmiliki wa duka hilo la dawa, ili kufahamu kabla ya kuingia nchini virusi vya corona bei ya barakoa na vitakasa mikono hivyo ilikuaje na kumchukulia hatua stahiki.