Wanaokwamisha ilani ya CCM wapewa onyo

0
198

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Mohamed Said Mohamed amewataka watendaji wa Chama hicho kusimamia miradi ya Serikali itekelezwe kwa wakati na kuonya yeyote atakaye kwamisha ilani ya Chama hicho ikiwemo miradi ya maendeleo kuchukuliwa hatua za kishereia.

Dkt. Mohamed Said Mohamed aneyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe ya Chama cha Mapinduzi katika viwanja vya Ruanda Nzovwe mkoani Mbeya zinazoangazia mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

Akiwa mgeni rasmi wa sherehe hizo ameagiza viongozi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa mbeya na mikoa iliyopojirani kuhakikisha wajumbe wa halmashauri kuu katika mikoa hiyo wanazitembelea wilaya zote, majimbo na kata zote za mikoa hiyo ili kueleza wananchi mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan

Sherehe ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mbeya imefanyika leo ili kuangazia miaka miwili ya mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.