Wananchi watakiwa kujitokeza kupata msaada wa kisheria

0
190

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, -Aboubakar Kunenge amefungua maadhimisho ya Wiki ya Sheria Kanda ya Dar es salaam, yanayofanyika pamoja na maadhmiisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu.

Kunenge amefungua maadhmisho hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa Wakazi wa jiji hilo kufika katika viwanja hivyo ili waweze kupata ushauri na msaada wa kisheria bila malipo.

Amesema miongoni mwa elimu itakayotolewa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria ni kuhusu taratibu za kufungua mashauri, sheria na taratibu zinazotumika katika kuendesha mashauri na elimu kuhusu taratibu za mashauri ya mirathi.

Mkuuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam amesema kuwa, Wananchi wataofika katika viwanja hivyo vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria watasikilizwa na kuhudumiwa.na jopo la Majaji, Wasajili, Naibu Wasajili, Mahakimu pamoja na Wadau wa Mahakama wakiwemo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria Kanda ya Dar es salaam pamoja na maadhmisho ya miaka 100 ya Mahakama Kuu yatafikia kilele chake tarehe 29 mwezi huu.

Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ni Mchango wa Mahakama katika kujenga nchi inayozingatia Uhuru, Haki, Udugu, Amani na Ustawi wa Wananchi.