Wananchi walalamika kuchapwa viboko

0
164

Wananchi wa Kijiji cha Saragulwa wilayani Geita wametaka kuchukuliwa hatua kwa Mtendaji wa kijiji hicho, Wasira Bulegi kwa madai kuwa amekuwa akiwachapa viboko pamoja na kuwalazimisha walipe faini ya mifuko ya saruji pindi wanapokiuka taratibu walizojiwekea katika kijiji hicho.

Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Ofisi za Afisa Mtendaji wa kijiji cha Saragulwa.

Akijibu malalamiko hayo mtendaji wa kijiji hicho ambaye ni mlalamikiwa
amekiri kumchapa viboko mwananchi mmoja ambaye alibainika kuiba mfugo.

Kufuatia tukio hilo, Magembe amemuonya mtendaji huyo kuacha tabia ya kuwachapa wananchi viboko na badala yake kufikisha mashauri yao katika mamlaka husika pindi wanapokosa.