Wananchi wa Msumbiji waendelea kupiga kura

0
173

Wananchi wa Msumbiji wanaendelea kupiga kura katika mchaguzi Mkuu, ambapo wanamchagua Rais wa nchi hiyo, Wabunge pamoja na Wawakilishi wa Serikali za Mitaa.

Rais Filipe Nyusi ambaye anawania kiti hicho kwa kipindi cha Pili, amepiga kura katika kituo kilichopo kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Maputo.

Awali akilihutubia Taifa kupitia Televisheni ya Taifa ya Msumbiji, Rais Nyusi amewataka Raia wa nchi hiyo kujiepusha va vurugu zozote wakati wa upigaji kura, wakati wa kusubiri matokeo na hata wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo.

Wakati zoezi la kupiga kura likiendelea nchini Msumbiji, vikosi vya ulinzi na usalama vimepelekwa katika jimbo la Cabo Delgado ambalo lina utajiri wa gesi lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo, ili kuzuia mashambulio ambayo yamekua yakifanywa na Wanamgambo.

Wanamgambo hao wa Al-Shabab ambao hata hivyo hawana uhusiano na Wanamgambo wa Al-Shabab wa nchini Somalia, wamekua wakifanya mashambulio hayo katika jimbo la Cabo Delgado tangu mwaka 2017 na wamekua wakishambulia zaidi vituo vya polisi na kuwaua kikatili raia pamoja na kuchoma moto nyumba zao.