Wananchi wa Chato wahimizwa kupanda miti kibiashara

0
173

Waziri wa Nishati ambaye pia ni mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani amewataka wananchi wa wilaya hiyo, kutumia fursa ya uwepo wa shamba la miti la Chato kujifunza njia bora ya kupanda miti kibiashara na kujiongezea kipato.

Akitoa salamu za wanachi wa wilaya hiyo katika hafla ya uzinduzi wa shamba la miti la Chato hii leo, Waziri Kalemani amesema uwepo wa shamba hilo ni fursa kwa wana Chato kujifunza na kuanzisha mashamba yao.

Dkt. Kalemani ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia utaalamu wa upandaji miti kutoka kwenye shamba hilo na kuanzisha mashamba yao ili kuwa na kilimo cha miti chenye tija.

“Nitoe rai kwa wananchi wa wilaya ya Chato kujifunza na kuanzisha mashamba yao kutokana na uwepo wa shamba hili kubwa Wilayani kwetu”,- amesema Dkt. Kalemani

Shamba la miti la Chato ni la pili kwa ukubwa katika mashamba 23 yanayosimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania-TFS.