Wanahabari wametakiwa kuwaelimisha Watanzania kuhusu mkataba wa uwekezaji wa bandari

0
126

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ametoa wito kwa Wahariri na Waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa wizara hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika mkoani Dar es Salaam, kwenda kuwaelimisha Wananchi kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam na kampuni ya DP World.

Profesa Mbarawa amesema kuwa, sio Wananchi wote wanaingia kwenye mitandao ya kijamii kuona yanayoendelea na kupata taarifa sahihi kuhusu mkataba huo, hivyo Wanahabari wana jukumu la kuwaelewesha na kuwaelimisha.

“Mkutano huu ni kutoa elimu na nyie ni watu muhimu sana katika nchi yetu. Tumetoa elimu na tutaendelea kutoa elimu. Sasa kazi yetu sisi kwa pamoja tuichukue elimu hii tuipeleke kwa Watanzania wengine”. Amesema Profesa Mbarawa na kuongeza kuwa

“Sisi tupo hapa kwa ajili ya kujenga Tanzania na kwa ajili ya maslahi ya Tanzania, na ndio sababu tumewaita hapa. Kazi kubwa baada ya kikao hichi mtoe ujumbe huu muende mkawaelimishe Watanzania”.