Wanafunzi wasioona nchini wakombolewa kitaaluma

0
142

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), imezindua rasmi kifaa kitakachomsaidia mwanafunzi asiyeona kusoma, kuandika na mchakato mzima wa ujifunzaji, ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Sense International Tanzania.

Kifaa hicho kinachoitwa Orbit Reader 20, kimezinduliwa Agosti 02,2021 mkoani Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dkt. Caroline Nombo amesema watoto wenye mahitaji maalum wanakabiliwa na changamoto katika kujifunza, hivyo kupatikana kwa Orbit Reader 20 kutasaidia wanafunzi wasioona kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema wanafunzi wasioona katika shule mbalimbali hawapaswi kuachwa nyuma na teknolojia.

” Teknolojia haichagui, hivyo uzinduzi wa kifaa hiki kutawafanya wawe sambamba na Teknolojia na kuleta matokeo chanya katika sekta ya Elimu,” amesema.