Wanafunzi wa darasa la Saba katika maeneo mbalimbali nchini wanaendelea na mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi iliyoanza mapema hii leo.
Mitihani hiyo inafanyika kwa muda wa siku mbili ambazo ni leo Septemba Tano na kumalizika siku ya kesho ambayo ni Septemba Sita.
Jumla ya watahiniwa 960,202 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo, watahiniwa wanaotoka katika shule 16,845.
Waandishi wa habari wa TBC katika maeneo mbalimbali nchini wamesema kuwa ulinzi umeimarishwa katika maeneo ya shule, na wanafunzi wanafanya mitihani hiyo katika mazingira ya utulivu.