Wanafunzi UDOM watakiwa kusoma kwa bidii

0
186

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Gaudentia Kabaka, ametoa wito kwa Wanafunzi wa Chuo hicho kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi mbalimbali.

Kabaka ametoa wito huo jijini Dodoma wakati wa Mahafali ya Kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), ambapo mgeni rasmi ni Rais John Magufuli.

Amesema kuwa, ni muhimu kwa Wanafunzi hao wanapokua chuoni wakazingatia masomo yao na kutambua kuwa Serikali pamoja na Wazazi wao wamekua wakipoteza fedha nyingi katika kuwasomesha.

Mwenyekiti huyo wa Baraza la Chuo cha UDOM ameongeza kuwa, kwa upande wake uongozi wa Chuo hicho utaendelea kuweka mazingira mazuri ili Wanafunzi hao waweze kufanya vizuri katika masomo yao.