Wanafunzi 3,000 wa shule za msingi Songwe hawajulikani walipo

0
154

Zaidi ya wanafunzi 3,000 katika shule za msingi mkoani Songwe waliotakiwa kuwa darasa la pili mwaka huu hawajulikani walipo.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Mkoa was Songwe, Michael Lugola katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Vwawa Day wilayani Mbozi kwa lengo la kujadili na kutathmini mwenendo mzima wa elimu

Lugola amesema mkoa wa Songwe una chagamoto ya utoro na mdondoko kwa wanafunzi, hali ambayo imechangia kuchochea mdororo wa elimu mkoani humo.

Ili kuhakikisha wanafunzi hao wanapatikana, Lugola amesema ushirikiano wa wazazi unahitajika ili kuwarudisha wanafunzi hao shuleni.

Katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa was Songwe, Omary Mgumba ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi amesema wadau wa elimu mkoani humo wanayo nafasi ya kuhakikisha wanatatua changamoto za elimu ili kuinua kiwango cha taaluma

Baadhi ya wadau wa elimu waliohudhuria kikao hicho wamesema njia bora ya kudhibiti utoro shuleni ni pamoja na kuwepo kwa chakula cha uhakika kwa wanafunzi.

Mkoa was Songwe uko unapakana na nchi mbili, ndiyo mkoa ambao zaidi ya asilimia 75 ya mizigo inayotoka Bandari ya Dar es Salaam inapita kuelekea nchi zilizopo Kusini mwa Afrika, hivyo umuhimu wa elimu kwa wanafunzi mkoani humo unahitajika