Wanafunzi 3 wafariki kwenye ajali ya moto

0
75

Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Buhangija manispaa ya Shinyanga wamefariki dunia, baada ya bweni walilokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio la moto huo ulioteketeza bweni la wasichana la shule hiyo.

Amesema moto huo ulianza kuwaka usiku wakati wanafunzi hao wamelala ndani ya bweni hilo, ambapo idadi yao walikuwa 32.

Kamanda Magomi amesema polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine wanaendelea na uchunguzi, ili kubaini chanzo cha moto huo.