Wanafamilia waliofariki ajalini waagwa

0
147

Miili ya ndugu watatu waliofariki katika ajali ya gari Agosti 02, 2023 Chalinze mkoani Pwani, ikiwasilishwa katika viwanja vya Gofu – Lugalo, Dar es Salaam kwa ajili ya kuagwa.

Ndugu hao ni Dkt. Norah Msuya, Sia Msuya na Diana Msuya ambao ni miongoni mwa ndugu wanne wa familia moja waliofariki katika ajali hiyo.

Ndugu mwingine aliyefariki dunia katika ajali ni kaka wa dada hao Neech Msuya ambaye alizikwa Agosti 6, 2023 kijijini kwao Msangeni, Ugweno wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Leo Agosti 08, 2023 dada hao watatu wanaagwa na mazishi yao yatafanyika katika makaburi ya Kondo, Ununio – Dar es Salaam.