Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi –CCM mkoa wa Njombe, Erasto Ngole amewataka wabunge na madiwani wa CCM mkoani humo kutumia muda uliobaki kabla ya uchaguzi mkuu kusahihisha malalamiko ya utendaji waliyonayo kwa wananchi.
Ngole ameyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo amesema chama hakitaweza kuteua wagombea ambao hawatatui kero za wananchi katika maeneo yao.
Akizungumzia uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa na vijiji Ngole amesema katika uchaguzi huo chama hakiwezi kubeba wagombea wanaotegemea rushwa.
Amesema chama kipo makini kuhakikisha wanapatikana wagombea ambao wataleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
