Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, – Constantine Kanyasu amewataka Wamiliki wa hoteli na sehemu za biashara za malazi nchini kuacha kuajiri vibarua, na badala yake waajiri Wafanyakazi wenye sifa stahiki watakaoweza kuwahudumia wateja wakiwemo Watalii.
Akizungumza katika mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Wawekezaji mkoani Morogoro, Naibu Waziri Kanyasu amewataka Wamiliki hao wasifikirie kujenga majengo mazuri ya hoteli bali pia wafikirie kuajiri Wafanyakazi waliosomea fani ya Utalii walio na sifa stahiki.
Ametolea mfano mkoa wa Morogoro ambao una hoteli nyingi nzuri, lakini zimekosa Wafanyakazi wenye sifa stahiki za kuhudumia Wateja, ambapo baadhi yao wanadaiwa kutokua na lugha nzuri na hawajui namna ya kupokea Watalii wanapofika katika hoteli hizo.