Walitumia ‘Finger Prints’ zako bila ya wewe kujua

0
231

“Tulikuwa na baadhi ya mawakala watoa huduma ambao hawakuwa waaminifu kwa maana ya kwamba wewe umeshafanya registration [usajili] na finger print [alama za vidole] yako umeondoka kumbe yeye aliendelea ku-register [sajili] namba nyingine kwa kutumia finger prints zako bila wewe kujua.

Baadaye hii namba inatumika kwenye uhalifu sasa baadaye unakuja kuunganishwa na wewe katika matukio ya uhalifu pasipo wewe kufahamu. Ndio maana tunasema hakiki kusudi zile namba ambazo huzifahamu maana yake hutozihakiki hivyo ikifika tarehe 13 hizo namba zitaondoka.”

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Bakari