Waliovamia makazi ya wazee kupelekwa mahakamani

0
260

Tulo Masanja Kamishna Msaidizi Ustawi wa Jamii Huduma kwa Wazee ameiambia TBC Taifa kuwa serikali imekwishaanza kuwapeleka mahakamani waliovamia kambi za makazi ya wazee.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza mapema leo Februari 25,2022 kupitia kipindi cha Mirindimo ya Asubuhi kilichokuwa kikifanyika katika kambi ya wazee Nunge Wilaya ya Kigamboni.

Aidha Masanja ameleza kuwa pamoja na kuwapeleka mahakamani wavamizi wa kambi hiyo bado serikali inampango na mikakati ya kuilinda kambi hiyo dhidi ya uvamizi ikiwa ni pamoja na kujenga uzio na kuendelea kuwapeleka mahakamani wavamizi wote wa kambi za wazee.

Akizungumza na TBC Taifa ametoa wito kwa jamii kuwasikiliza wazee nakuwajali akikumbusha kuwa wazee ni tunu ya taifa kwani wanastahili kurudishiwa fadhila baada ya kulitumikia taifa lao.

Sambamba na hii ameileza TBC Taifa kuwa ipo haja ya kuwatumia wazee kupata elimu kwani wapo na ujuzi ambao jamii inapaswa kurithishwa, akitoa mfano kuwa wapo wazee waliotoka Tanga ambao waliingia nchini wakijihusisha na kilimo cha mkonge hivyo ni vyema elimu hiyo ingerithishwa kwa jamii.

“Kuna wazee wapo Tanga walikuja zamani wakati wakukata Mkonge miaka ya 70 na walitoka kwenye mikoa ya mbali wakatengeneza familia, wakati mwingine wanaujuzi wa thamani na moja wa watu walisema ujuzi hauzeeki sasa anataamani kushae ujuzi wake na jamii ila wakati mwingine jamii haipo karibu na wazee” amesema

Mmoja wa wazee aishie katika kambii hii anayefahamika kwa jina la Nuru Saidi ameeleza kuwa athari wanayokutana nayo kutokana na uvamizi wa makazi yao ni kukosa maeneo ya kulima mboga mboga kwaajili ya chakula.

“Watu wanachimba misingi na kujenga wakiandikiwa bomoa mara moja wanafuta wanaendelea kujenga pia nahofia makazi yetu yakizidi kuvamiwa sasa tutakosa hata pakulima mboga” ameeleza

Veronica Msanjira Afisa ustawi wa jamii msaidizi kata ya Vijibweni ameeleza kuwa uvamizi umepelekea eneo hilo la kambi ya wazee kupungua kutoka hekari 50.8 nakubakia hakari 25 akisisitiza kuwa iwapo wavamivi hawatazibitiwa wanaweza kulitwaa eno lote kwani tayari wanekwisha anza kujenga nyumba katikati ya kambi.

“Mwaka 2015 manispaa ya Temeke ilikuja kupima ikakuta zimabakia takribani hekari 25 ambapo sasa watu wanaendela kuvamia ndani ya haya makazi wanashambulia eneo lililobakia” ameeleza

Mkazi wa Vijibweni Zawadi Juma amesema kuwa ili suluhu ipatikane Serikali isilifumbie macho jambo hili la uvamizi na kwa wale wenye mgogoro na uongozi wamelize migogoro ili wasiwe na kisingizio cha kuvamia kambi hii.