Waliouawa Watanzania Sita wasakwa

0
166

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz amesema kuwa, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama litahakikisha linawakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria watu wote waliohusika na mauaji ya Watanzania Sita mkoani Mtwara.

Mauaji hayo yametokea hapo jana katika kijiji cha Ngongo wilayani Tandahimba, ambapo Watanzania hao waliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji.

Katika tukio hilo, watu wengine Watano wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Kufuatia tukio hilo, DCI Boaz ametoa wito kwa Watanzania wote wanaotaka kusafiri kwenda nje ya nchi kuhakikisha wanakuwa na vibali stahiki.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo kutoka Jeshi la Polisi nchini Liberatus Sabas amesema kuwa, Serikali haitakubali kuona Raia wake wasio na hatia wanapoteza uhai kwa sababu ambazo hazifahamiki.