Waliouawa Kigoma wazikwa

0
115

Miili ya watu sita wa familia moja waliouawa kwa kukatwa na kitu kinachodaiwa kuwa na ncha kalli, imezikwa katika kijiji cha Kiganza wilayani Kigoma mkoani Kigoma.

Habari kutoka mkoani Kigoma zinaeleza kuwa, miili hiyo imezikwa kwa pamoja jana Jumapili majira ya usiku.

Watu hao waliuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wakiwa nyumbani kwao wamelala, huku watoto wawili wakijeruhiwa.

Kaimu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema jeshi hilo linaendelea na msako ili kuabaini watu waliofanya ukatili huo pamoja na kufahamu chanzo chake.

Watoto waliojeruhiwa katika tukio hilo wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kigoma – Maweni.