Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam imewafutia mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa Watano waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.
Uamuzi huo umetolewa hii leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, -Thomas Simba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Walioachiwa huru ni Audai Ismail, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika kosa la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).