Wakuu wapya wa wilaya watakiwa kuchapa kazi

0
180

Mkuu wa mkoa wa Mara, Ally Hapi amewataka wakuu wapya wa wilaya za mkoa huo kuchapa kazi, ili kuusaidia mkoa kuzidi kupiga hatua kimaendeleo.

Hapi ametoa kauli hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya walioteuliwa hivi karibuji na Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema wakuu hao wa wilaya wana jukumu kubwa la kujenga Mara mpya iliyobeba maono na mabadiliko makubwa ya kiuchumi.

Hapi pia ametoa msisitizo katika sekta ya elimu na kusema kuwa mkoa wa Mara uko nyuma na hauridhishi kwenye matokeo kwa shule za msingi na sekondari, hivyo ni jukumu lao kuhakikisha wanasimamia na kutatua matatizo yote sugu ndani ya sekta ya elimu.