Wakuu wa Taasisi za kupambana na rushwa Barani Afrika, watatembelea vivutio vya Utalii vilivyopo katika mikoa ya Arusha na Manyara Julai 13, 2023 baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya Siku ya Kupambana na Rushwa Afrika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene wakati akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo yanayofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku tatu.