Mkurugenzi wa Huduma na Usimamizi kutoka @wizara_ya_kilimo Kemilembe kafanabo ametoa wito kwa Wakulima wa zao la chai nchini kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF)
ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni mkoani Dar es Salaam.
Kemilembe amewasisitiza Wakulima kuchangamkia fursa hiyo kwani watapata taarifa mbalimbali kuhusu soko la zao la chai.
“Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika (African Food System Forum) unaleta shauku na hamasa kubwa kwa wazalishaji na wauzaji wa chai kupata taarifa mbalimbali zitakazochochea zao hilo kupata mapato zaidi,” amesema Kemilembe
Pia ametoa wito kwa Wakulima wa chai nchini kuzingatia uzalishaji wa chai unaokidhi viwango na ubora wa Kimataifa, ili kukuza soko la bidhaa hiyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo wa Huduma na Usimamizi kutoka @wizara_ya_kilimo amesema vipaumbele vya vya sasa vya kuchochea uzalishaji na mauzo ya zao la chai ni pamoja na kuhamasisha, kusimamia na kudhibiti uzalishaji ili kuongeza ubora wa chai unaokidhi viwango vya soko Kimataifa.
Kwa mujibu wa takwimu za @wizara_ya_kilimo,uzalishaji wa zao la chai umeongezeka kutoka tani elfu 24.8 mwaka 2021/2022 hadi kufikia tani elfu 26.75 kwa mwaka 2022/2023 ambapo jumla ya tani elfu 21.09 zimeuzwa nje ya nchi.