Wakristo washerehekea Pasaka

0
436

Watanzania wameshauriwa kuendelea kulinda amani na kudumisha mshikamano, kwa kuwa mambo hayo ni silaha pekee kwa Taifa kupata maendeleo.

Ushauri huo umetolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga mkoani Kagera,- Almachius Rweyongeza wakati wa Misa ya Pasaka Kitaifa iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu George Jimbo Katoliki la Kayanga wilayani Karagwe.

Ameongeza kuwa amani ni matunda ya haki, hivyo jamii na serikali kwa ujumla wanapaswa kuwajibika na kila mmoja kubeba majukumu yake kama alivyofanya Yesu Kristo.