Wakazi wa Nkasi wamsubiri Rais

0
247

Wakazi wa mji wa Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa kwenye uwanja wa Sabasaba, wakimsubiri Rais John Magufuli ambaye anatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara hii leo.

Shughuli nyingine aliyoifanya Rais Magufuli akiwa wilayani Nkasi, ni kutatua mgogoro wa ardhi kati ya Wananchi wa kijiji cha Kalongwe, kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Kituo cha Utafiti wa Kilimo – Uyole.

Katika kutatua mgogoro huo , Rais Magufuli ameagiza JKT wabaki na Ekari Elfu 22, Chuo cha Uyole Ekari Elfu Tano na Ekari Elfu Moja zirudi kwa Wananchi.