Wakazi Shinyanga waiomba Serikali kukarabati Barabara

0
157

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwakitolyo wilayani Shinyanga, wameiomba serikali kusaidia kutengeneza barabara inayonganisha wilaya za Shinyanga na Kahama, kufuatia barabara hiyo kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Shinyanga.

Wakazi hao wamesema hivi sasa inawalazimu kuvuka kwenda wilaya ya Kahama kwa kutumia Mitumbwi hali inayohatarisha usalama wa maisha yao.

Hivi sasa wananchi wanaotumia barabara hiyo wanalazimika kutumia mitumbwi ili waweze kuvuka na kuendelea na safari zao jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa mali na maisha yao.

Hata hivyo Shughuli kadhaa za kiuchumi na kijamii zimesimama hali inayowafanya wananchi kutaabika zaidi.

Kaimu mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga, Elias Matijo amesema Jeshi la Polisi linahakikisha usalama wa wananchi wanaotumia barabara hiyo unaimarika.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akawaomba Wananchi hao kuwa na subira wakati serikali inafanya mchakato wa kutengeneza Barabara hizo.