Wakandarasi watakiwa kufanya kazi kwa viwango

0
183

Wakandarasi wa mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini waliopewa dhamana ya kufanya kazi na serikali wametakiwa kufanya kazi Kwa viwango ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu imara itakayotumia vifaa vyenye ubora.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy wakati wa makabidhiano ya mikataba ya usamabazaji wa umeme mkoa wa Tanga.

Jumla ya shilingi bilioni 76.9 zimetolewa kwenye mikoa nane ili kujenga miundombinu ya umeme kwenye vijiji vilivyopo pembezoni ikiwemo mkoa wa Tanga ambao umepata shilingi bilion 11.