Wakamatwa wakitorosha dhahabu

0
175

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata raia wawili wa China na Mtanzania mmoja aliyewekeza katika machimbo ya madini wilayani Ulanga, kwa tuhuma za kujaribu kutorosha kilo mbili za dhahabu zenye thamani ya shilingi milioni 337.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, – Fortunatus Musilimu amethibitisha kukamatwa kwa watu hao.

Kamanda Musilimu amesema uchunguzi wa kina unaendelea, na kwamba watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa.

Amesema uongozi wa wilaya ya Ulanga ulipata taarifa za utoroshaji wa madini hayo yaliyochimbwa katika mgodi uliopo kwenye kijiji cha Isyanga, na walipofuatilia ndipo waliwakamata watuhumiwa hao.