Waitara : Msikosoe teuzi za Rais

0
200

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara amewataka Viongozi, Watumishi na Wananchi wa wilaya ya Rorya mkoani Mara kuacha tabia ya kukosoa teuzi za Rais alizozifanya kwa baadhi ya Viongozi.

Waitara ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha viatu kilichopo Kijiji cha Nyanchabakenye wilayani humo na kuongeza kuwa kumekuwa na tabia miongoni mwa Viongozi, Watumishi na Wananchi wilayani Rorya kukosoa teuzi zinazofanywa na Rais kwa Viongozi wanaopangiwa kazi wilayani humo, tabia ambayo haipendezi.

Amesema Viongozi, Watumishi na Wananchi hawana mamlaka ya kusema nani wanayemtaka awaongoze, hivyo ni vema kuheshimu maamuzi ya Rais katika teuzi zake kwani ndiye mwenye mamlaka ya kuteua kulingana na sifa za kiongozi.