Wahitimu wa vyuo vya mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) wamedhihirisha kwa vitendo kuwa elimu waipatayo vyuoni humo inawawezesha kutatua changamoto mbalimbali za kijamii kwa kutengeneza mashine mbalimbali.
Hayo yamebainika katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya mashine tano za kuchanganya madini joto kwenye chumvi zilizotengenezwa na wahitimu wa VETA.
Makabidhiano haya yamefanyika kati ya Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (OR-TAMISEMI)