Idara ya uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam imefanikiwa kuwakamata wahamiaji Haramu 90 waliokuwa wakiishi hapa nchini kinyume na sheria.
Wahamiaji hao haramu 54 ni kutoka nchini China huku Raia kutoka mataifa kama India, Misri, Philippines, Malawi, Kenya na DRC wakiwa ni miongoni mwa waiokamatwa kati ya Juni mosi na Juni saba mwaka huu.
Kaimu Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Eliza Luvanga amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa baada ya kukamatwa kwa wahamiaji hao ikiwa ni pamoja na kuwalipisha ada za vibali vya kuishi hapa nchini na faini za ukimbizi haramu.
Aidha Luvanga ametoa onyo kali kwa watanzania wanaowahifadhi wahamiaji haramu katika maeneo yao kwani mkono wa sheria unaweza kuwafikia na kuhukumiwa mpaka miaka 20 jela.