Wagonjwa wengine wa Corona wapona

0
580

Mapema mchana wa leo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametangaza kuwepo kwa wagonjwa wawili, kutoka Arusha na Dar es Salaam wamepona.

Kupona kwa mgonjwa huyo wa Arusha kumeufanya mkoa huo kukosa mgonjwa mwingine wa Corona.

Jumla ya visa vilivyothibitishwa Tanzania hadi kufikia leo ni 24, watano wamepona na kifo ni kimoja.