Wafanyakazi washerehekea Mei Mosi

0
392

Maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi Kitaifa katika viwanja vya Sokoine mkoani Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Wafanyakazi nchini, leo wanaungana na wenzao wa nchi mbalimbali duniani kusherehekea Sikukuu ya Wafanyakazi – Mei Mosi.

Sherehe za Mei Mosi Kitaifa kwa mwaka huu zinafanyika mkoani Mbeya na Mgeni rasmi atakua Rais John Magufuli ambaye tayari yupo mkoani humo akiendelea na ziara yake ya kikazi ya siku Nane.

Kaulimbiu ya Kitaifa ya Sikukuu ya Mei Mosi kwa mwaka huu ni “Tanzania ya Uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya Wafanyakazi ni sasa”.

Wakati wa Sikukuu ya Mei Mosi, Wafanyakaza kutoka sekta mbalimbali wanaungana na kutathmini utekelezaji wa majukumu yao katika sehemu zao za kazi pamoja na kuyjadili njia za kutatua changamoto zinazowakabili.