Wadau waungana kukabili mabadiliko ya tabianchi kwa afya

0
341

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amezindua Umoja wa  Kukabili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi kwa Afya ya Mama na Mtoto huku akisistiza kuwa utasaidia kuikoa maisha ya kada hiyo ya Jamii.

Umoja huo umezinduliwa  katika Makazi ya Balozi wa Uingereza mkoani Dar es Salaam na utasimamiwa na Taasisi ya Doris Mollel.

Umoja huo ambao ni wa kwanza wa namna yake nchini katika sekta ya afya, umelenga kuwa mstari wa mbele katika kufanya tafiti, kuelimisha jamii na kuleta pamoja serikali, sekta binafsi, na asasi za kimataifa katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Akiwakaribisha wageni waalikwa katika makazi ya Balozi wa Uingereza Nchini, Mkurugenzi wa Maendeleo wa Ubalozi huo Eduarda Gray, ameipongeza Doris Mollel Foundation kwa hatua hiyo kubwa na kuahidi ushirikiano na Taasisi hio.

Uzinduzi huo umehusisha wadau kutoka UNICEF, UNEP, Save the Children, Ofisi ya Makamu wa Rais, Vodacom Tanzania, na Sharon Ringo Foundation.