Wadau wa uchaguzi watakiwa kushirikiana na NEC

0
351

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amewataka wadau wa uchaguzi nchini kuendelea kushirikiana na tume hiyo ili iweze kufanikisha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Jaji Mstaafu Kaijage amesema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na wadau wa uchaguzi wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya siasa nchini, kwa lengo la kuwaelezea kuhusu awamu ya kwanza ya uboreshaji wa dafatari la wapiga kura na maandalizi ya awamu ya pili ya uboreshaji wa daftari hilo.

Akiwasilisha mada inayohusu awamu ya kwanza ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt Wilson Charles amesema, licha ya mafanikio waliyoyapa katika, walikutana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na baadhi ya maeneo kutofikika kirahisi na wananchi kusubiri siku ya mwisho ya uboreshaji huo, hali iliyosababisha msongamano.

Kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu, NEC imeendelea kukutana na wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa, ili kujadiliana mambo mbalimbali.