Wabunifu na wavumbuzi waendelezwe

0
89

Serikali imejipanga kukuza vipaji vya wabunifu na wavumbuzi wa ndani, lengo likiwa ni kuleta maendeleo chanya kwaTaifa.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa wiki ya Tafiti na Ubunifu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga amesema tayari serikali imeweka vipaumbele vya kitafiti kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Amesema lengo la tafiti hizo ni kuibua bunifu na teknolojia zinazozalishwa na wabunifu na wavumbuzi wa Kitanzania watakaoweza kuitanganza nchi kimataifa kwa kazi bora.

Naibu Waziri Kipanga amebainisha kuwa mkopo wa elimu ya juu ulioongezwa hadi kufikia shilingi bilioni 570 , unatarajiwa kufika shilingi bilioni 700, kwa kuwa benki ya NMB nayo itaongeza shilingi bilioni 200.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema, chuo hicho kimejipanga kuhakikisha kinazalisha wataalamu wa kutosha kukidhi mahitaji ya nchi si tu kielimu bali pia kwenye sayansi, teknolojia na bunifu

Jumla ya wabunifu na wavumbuzi 1,785 wametambuliwa na serikali ndani ya kipindi cha miaka mitatu kupitia mchakato wa mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU).

Wabunifu 200 kati ya hao tayari wameendelezwa.